Local Bulletins

Hatimaye bomu lililopatikana katika eneo la Sowit kaunti ya Samburu lateguliwa.

Bomu lililopatikana katika eneo la Sowit kaunti ya Samburu.
Picha:Hisani

By Waihenya Isaac,

Wakaazi wa eneo la Shabaa kaunti ndogo ya Samburu ya kati wamepata afueni baada ya bomu lililopatikana katika eneo la sowit siku ya ijumaa kuteguliwa.

Bomu hilo lilipatikana likiwa limefukiwa kwenye mchanga na watoto waliokuwa wakichunga mbuzi karibu na nyumba yao.

Maafisa wa polisi wakiongozwa na naibu kamanda wa kaunti ya Samburu Abdikadir Malicha walitegua bomu hilo baada ya kulilinda siku nzima.

Polisi wamewataka wenyeji kutoa taarifa mara kwa mara wanapota vyuma ambavyo havieleweki.

Subscribe to eNewsletter