Local Bulletins

Shirika La Haki Afrika Laitaka NCIC Kufunganya Virago Vyake Iwapo Haitawajibika Katika Kudhibiti Mihemko Ya Kisiasa Na Malumbano Nchini.

 

Picha;Hisani

By Adano Sharawe,

Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu nchini Haki Afrika linaitaka Tume ya uiano na utangamano wa kitaifa-NCIC kufunganya virago vyake iwapo haitawajibika katika kudhibiti mihemko ya kisiasa na malumbano makali nchini.

Afisa wa maswala ya dharura wa Shirika hilo Mathias Shipetta amesema Tume hiyo imeshindwa kuwakabili ipasavyo wanasiasa au hata kushirikiana na taasisi nyinginezo katika kuwaadhibu ipasavyo.

Shipetta amesema ni sharti Tume hiyo iwajibike hasa wakati huu uchaguzi mkuu unapokaribia la sivyo ifunganye virago na kuondoka mamlakani.

Shipetta aidha amekosoa Tume hiyo kwa kusalia kimya licha ya kuwaona wanasiasa wakiwagawanya Wakenya katika misingi ya kikabila.

Kauli ya Shipetta inajiri huku Tume hiyo ikiwaorodhesha Wanasiasa Mike Mbuvi Sonko, Simba Arati, Silvanus Osoro na Johanna Ng’eno kama wasiyofaa kuwa viongozi kutokana na tabia zao mbovu na ukosefu wa maadili.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter