Local Bulletins

Chama cha ODM kitafanya mchujo wa haki na usawa. – Katibu mkuu Edwin Sifuna.

Katibu mkuu wa Chama cha ODM Edwin Sifuna.
Picha:Hisani

Na Waihenya Isaac,

Chama cha ODM kitafanya mchujo wa haki na usawa.

Hayo ni kwa mujibu wa katibu mkuu wa chama hicho Edwin Sifuna.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya mkutano na viongozi wa chama hicho,Sifuna ametaja kuwa chama hicho kitanzingatia usawa chamani bila mapendeleo.

Aidha Sifuna amekariri kuwa wanachama wote chamani humo wana haki sawa bila kujali muda waliojiunga na chama hicho cha Chungwa.

Ametaja kuwa chama hicho kitawania viti vyote vya uwakilishi nchini na pia kitasimamisha wagombea kila pembe ya nchi katika uchaguzi mkuu ujao.

Vyama vya kisiasa hukumbwa na wakti mgumu haswa baada ya shughuli za mchujo baada ya wasio ridhika na shughuli hiyo kuhamia vyama pinzani Jambo ambalo kila chama kinajiza titi kuzuia wakti huu taifa linapoelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter