Local Bulletins

Bunge La Kitaifa Liko Tayari Kuandaa Mswaada Wa Kura Ya Maamuzi Na Marekebisho Ya Katiba BBI.

Bunge La Kitaifa.
Picha;Hisani

 

By Waihenya Isaac

Kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Amos Kimunya amesema kuwa Bunge liko tayari kuandaa mswaada wa kura ya maamuzi na marekebisho ya katiba huku kaunti zikitarajiwa kuwasilisha matokeo ya kura ya mswaada wa BBI wiki ijayo.

Akizungumza na waandishi wa habari,Kimunya ametaja kuwa kesi iliopo mahakamani ya kutaka kusitishwa kwa kura ya maamuzi haitazuia Bunge hilo kuendelea na kazi yake ya ukarabati wa Katiba.

Kimunya ametaja kuwa Bunge hilo likagua namna Mabunge ya kaunti yalivyohusisha umaa na kupata maoni kutoka kwa umaa kabla ya kuupitisha mswaada huo.

Aidha shughuli sawia na hiyo itandaliwa pia na Bunge la kitaifa kabla ya kuujadili mswada huo Bungeni.

Kufikia sasa mabunge 41 ya kaunti yamepitisha mswada huo, huku Bunge la Kaunti ya Baringo likiwa la kipekee lililoukataa.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter