Local Bulletins

BBI Si Tiba Kwa Changamoto Za Kisiasa Nchini. – Linda Katiba.

Picha; Hisani

By Samuel Kosgei,

VUGUVUGU linalopinga marekebisho ya katiba, limetaja uhasama ulioibuka kati ya wanachama wa ODM na serikali ya Rais Uhuru Kenyatta kama ishara kuwa Mpango wa Maridhiano (BBI) si tiba kwa changamoto za kisiasa nchini.

Vuguvugu hilo la Linda Katiba linalojumuisha viongozi wa kisiasa na wa mashirika ya kutetea haki za raia, imeshikilia kuwa mapendekezo ya kurekebisha katiba kupitia kwa BBI yatanufaisha viongozi wachache pekee.

Msimamo wa viongozi hao wakiwemo Kiongozi wa Narc-Kenya, Bi Martha Karua, mtaalamu wa masuala ya uchumi, Dkt David Ndii, aliyekuwa Jaji Mkuu Willy Mutunga na wengine, ni tofauti na waasisi wa BBI.

Kwa mujibu wa wanaounga mkono marekebisho ya katiba yanayopigiwa debe na Rais na waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga, mapendekezo ya kurekebisha katiba yatatoa nafasi ya kuwepo waziri mkuu na manaibu wake, na pia kumpa mamlaka kiongozi wa huyo.

Chama tawala cha Jubilee kimeandikia barua bunge likisema kuwa litawasilisha mapendekezo na maoni yake kuhususia na mchakato wa BBI wakti wananchi watakapotoa maoni yao kwenye harakati za kuhusisha umma.

Katibu wa chama hicho Raphael Tuju amesema kuwa chama chao kitajifikisha bungeni mbele ya kamati za sharia za bunge la seneti na lile la kitaifa hapo kesho alhamisi.

Mabunge hayo mawili yanapania kuendesha shughuli ya kuchukua maoni ya umma kwenye mchakato wa kufanikisha BBI.

Hii inajiri baada ya maspika wa mabunge yote yote mawili kupokea vyeti vya kupitishwa kwa BBI katika mabunge ya kaunti Zaidi ya 24 kama inavyohitajika kikatiba.

 

Subscribe to eNewsletter