Local Bulletins

Asilimia 70 Ya Vijana Nchini Watapiga Kura Kuangusha Mpango Mzima Wa (BBI) Ikiwa Ingefanyika Leo Huku Asilimia 30 Wakiunga Mkono.

Picha:Hisani

By Samuel Kosgei,

Utafiti mpya uliofanywa sasa unaonesha kuwa asilimia 70 ya vijana nchini watapiga kura kuangusha mpango mzima wa (BBI) ikiwa ingefanyika leo huku asilimia 30 wakiunga mkono.

Utafiti huo uliotolewa na Taasisi ya Emerging Leaders Foundation (ELF) Afrika, umefichua kuwa asilimia 40 wavulana wataipinga huku asilimia 21 wakiunga mkono. Asilimia 30 ya wasichana wangeipinga huku asilimia 9 wakiunga mkono kura hiyo ya BBI.

Asilimia 70 ya washiriki wa Utafiti huo wamesema hawakupata nafasi kivyao au kupitia mashirika yao kutoa maoni  au kuhusishwa kwenye mchakato mzima wa BBI na jopo lililokuwa likichukuwa maoni.

Asilimia 50 wamesema kuwa wamesoma ripoti ya BBI, asilimia 12 wamesema hawajasoma huku asilimia 38 wakisema wamesoma kurasa kadhaa za mswada huo .

Asilimia 54 ya waliohojiwa walisema walipata ripoti ya BBI kwenye WhatsApp, asilimia 18 kwenye Twitter, asilimia 5 kwenye Facebook, asilimia 4 kwenye Barua pepe, asilimia 10 wana nakala yenyewe huku asilimia 9 hawajaiona hata kidogo.

Kulingana na ripoti hiyo, asilimia 47 ya waliohojiwa wanadhanai  ripoti hiyo ya BBI haina manufaa yoyote kwa vijana huku asilimia 8 tu wakiwa na Imani nayo.

Hayo yanajiri huku bunge la kaunti ya Siaya likipitisha mswada huo wa BBI hii leo.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter