Local Bulletins

Aliyekuwa Mbunge wa Samburu Mashariki Job Kasaine Lalampaa azikwa hii leo.

Hafla ya mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Samburu Mashariki Job Kasaine Lalampaa katika kijiji cha Ldupai Samburu mashariki.
Picha; Silvio Nangori.

Na Silvio Nangori,

Aliyekuwa Mbunge wa Samburu Mashariki Job Kasaine Lalampaa amezikwa hii leo nyumbani kwake katika kijiji cha Ldupai Samburu mashariki.

Kasaine alikuwa Mbunge wa Samburu Mashariki Tangu mwaka wa 1979 Hadi 1992.

Alikuwepo miongoni mwa viongozi walitajwa kufanya Maendeleo mengi katika kaunti hiyo.

Kasaine alichaguliwa kama Mbunge wa Samburu mashariki mwaka wa 1979 na kuwa uongozini kwa takriban miaka 15.

Aliteuliwa kama Naibu waziri wa Biashara wakati wa uongozi wa Hayati Daniel Toroitich Arap Moi.

Wenyeji na viongozi katika kaunti ya samburu wamemtaja Kasaine kama kiongozi aliyesaidia katika kuleta Amani katika kaunti ya Samburu na vile vile kuipa  jamii ushauri kuhusu umuhimu wa Elimu.

Mwendazake Aliaga Dunia tarehe 6 mwezi huu wa Mei akiwa anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Kenyatta jijini Nairobi baada ya kuugua kwa Muda mrefu.

Ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 76.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter