Local Bulletins

Aden Duale si msemaji wa wafugaji asema Mbunge Alois Lentoimaga wa Samburu Kaskazini

Mbunge Samburu Kaskazini Alois Lentoimaga. Picha, hisani.

Na Silvio Nangori

Aliyekuwa kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale ameonywa dhidi ya kuzungumza kwa niaba ya wafugaji humu nchini.

Akizungumza na wanahabari Mbunge wa Samburu Kaskazini Alois Lentoimaga na ambaye ni wenyekiti ya jamii ya wafugaji amesema kwamba Duale amekosea heshima jamii za wafugaji kwa kuwajumlisha katika mazungumzo yake.

Lentoimaga ametoa ushauri kwa jamii ya wafugaji humu nchini kujiepusha na viongozi wanaochangia katika migawanyiko yao na vile vile kwa ajili yao binafsi.

Aidha amesema kwamba wabunge kutoka kwa jamii ya wafugaji walipiga kura bungeni kwa pamoja kumuondoa Duale kama kinara wa wengi.

Comments are closed.

Subscribe to eNewsletter