Local Bulletins

Watu wawili wauawa katika mapigano Marsabit

OCPD wa Marsabit ya kati Benjamin Mwanthi aliyethibitisha mauaji hayo.

Watu wawili wameaga Dunia kufuatia mapigano mapya kati ya jamii mbili katika Eneo La Gof Choba kaunti hii ya Marsabit.

Akidhibitisha kisa hicho, OCPD wa Marsabit ya Kati Benjamin Mwanthi amesema hali ya utulivu imerejea kwa sasa huku maafisa wa usalama wametumwa ili kushika doria.

Polisi waliarifiwa mida ya saa kumi alasiri ambapo walifika eneo la tukio na kupata miili ya wahasiriwa ambao wote ni wanaume wa umri wa makamo.

Japo kiini cha mapigano hayo haikujulikana mara moja, Mwanthi amesema mzozo wa mipaka na malisho ambao umekuwa ukitokota kwa muda wa wiki moja sasa huenda ukafufua mapigano hayo mapya.

Mwanthi amehakikishia wananchi kuwa serikali itaimarisha usalama na amezitaka jamii zinazozana kusitisha uhasama na kuzingatia amani.

Aidha, amewataka wanasiasa jimboni kukoma kuchochea wananchi kupigana.

Subscribe to eNewsletter