Local Bulletins

Watu 317 Hapa Nchini Hujitoa Uhai Kila Mwaka.

Katibu Wa Utawala Katika Wizara ya Afya Rashid Aman.
Picha; Hisani

Wizara Ya Afya Imeweka Wazi Kuwa Watu 317  Hapa Nchini Hujitoa Uhai Kila Mwaka, Huku  Taifa La Kenya Likishikilia Nafasi Ya 114 Ulimwenguni Kati Ya Mataifa 175 Kwa Visa Vya Kujitoa Uhai Kutokana Na Sababu Mbalimbali.

Akizunguzumza Akiwa Katika Hospitali Ya Wagonjwa Wa Akili Ya Mathare Jijini Nairobi, Katibu Wa Utawala  Katika Wizara Ya Afya Daktari Rashid Aman Amesema Kuwa, Kati Ya Mwaka Wa 2008 Na 2017 Taifa Lilirekodi Ongezeko La Visa Vya Kujitoa Uhai Hadi Asilimia 58.

Hospitali Ya Wagonjwa Wa Akili Ya Mathare Jijini Nairobi.
Picha; Hisani

Vifo Hivyo Vimetajwa Kusababishwa Na Mambo Tofauti Ikiwemo Msongo Wa Mawazo Na Mizozo Ya Kifamilia.

Aidha Vijana Wa Kati Ya Umri Wa Miaka 15 Hadi 29 Wametajwa Kuadhirika Zaidi.

Aman Amesema Kati Ya Watu Laki Moja Humu Nchini Asilimia 6.5 Wanadaiwa Kuugua Maradhi Ya Akili Yanayochangia Wengi Wao Kujitoa Uhai.

Vilevile Aman Amesemakuwa  Madaktari 48 Wa Akili Wanatarajiwa Kutumwa Katika Kaunti Zote Humu Nchini Ili Kuwashughulikia Wagonjwa Wa Akili.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter