Local Bulletins

Uvamizi wa majambazi kule Hulahula wawajeruhi ng’ombe kwa risasi

Na Adho Isacko

Kundi la majambazi wasiojulikana siku ya Jumatano walivamia mifugo ya wakaazi wa eneo la hulahula katika msitu wa Marsabit saa sita mchana na kujeruhi ngombe 3.

Kulingana na aliyeshuhudia tukio hilo Bileua Keina majambazi hao ambao walikua na bunduki walifika katika eneo la wortikele ambapo mifugo hunywa maji na kupiga risasi kadhaa huku wakiwatawanya ng’ombe hao.

Wakaazi wa eneo hilo waliposikia risasi walikimbia kusaidia waliokuwa wakichunga ng’ombe hao na kuweza kuwarejesha.

Wakaazi hao wamewasuta maafisa wa polisi kwa kufika kwenye eneo hilo wakiwa wamechelewa.

Juhudi zetu za kupata ripoti zaidi kutoka kwa OCPD wa Marsabit David Muthure hazikufua dafu kwani hakuwa ofisni mwake na wala hakupokea simu zetu.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter