Local Bulletins

Tahadhari zaidi bado virusi vya corona vipo, yasema serikali

Na Adho Isacko

Na Adho Isacko

Wananchi wamehimizwa kuendelea kufuatia maagizo ya serikali kwani ugonjwa wa covid-19 una hatua tofauti na unaweza anza tena.

Akizungumza Jumanne kwenye jumba la afya katibu wa utawala katika wizara ya afya Dkt Rashid Aman amesema kuwa hata kama idadi inaonekana kupungua, kuna kaunti kama vile machakos ambayo inaendelea kurikodi idadi ya juu na hivyo ni vyema kuzingatia masharti zote.

Amepeana mfano wa nchi zingine ambazo zilifungua uchumi baada ya idadi kupungua na watu kupuuza maagizo ya serikali, hiii ikasababisha vifo zaidi na kulazimu serikali kufunga tena.

Watu wengine 151 wamepatikana na virusi vya korona  bada ya sampuli 2,552 kupimwa katika saa 24 zilizopita .

Idadi hiyo sasa   inafikisha  jumla ya visa vya ugonja huo nchini kuwa elfu 35,335 baada ya jumla ya vipimo elfu 47,9697 kufanyiwa vipimo.

Kwenye hotuba ya kila siku kuhusu hali ya maambukizi nchini,katibu wa utawala katika wizara ya afya Rashid Aman amesema  kati ya walioambukizwa ugonjwa huo  77 ni wanawake na 74 ni wanaume.

Kwa mara ya kwanza idadi ya wanawake waliopata ugonjwa huo imezidi ile ya wanaume  wote walioambukizwa ugonjwa huo ni wakenya isipokuwa watu wawili .

Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 3 ilhali wa umri wa juu ana miaka 74.

Watu wengine 173 wamepona na kufikisha jumla ya waliopona ugonjwa huo kuwa 21483 huku pakiwa hakuna aliyeaga dunia kwa ajili ya virusi hivyo katika saa 24 zilziopita na kufanya idadi ya walioaga dunia kusalia 599.

Aidha aman amehimiza  wananchi kuendelea kufuatia maagizo ya afya ili kujizuia dhidi ya ugonjwa wa covid-19.

Subscribe to eNewsletter