Local Bulletins

Spika Wa Bunge La  Seneti Ken Lusaka  Kupokea Azimio La Bunge La Kaunti Ya Nairobi La Kumbandua Gavana Wa Nairobi Mike Sonko Mamlakani

Picha: Hisani

By Waihenya Isaac,

Spika Wa Bunge La  Seneti Ken Lusaka  Anatarajiwa Kupokea Azimio La Bunge La Kaunti Ya Nairobi Kupitisha Hoja Ya Kumuondoa Mamlakani Gavana Wa Nairobi Mike Sonko.

Hii Ni Baada Ya Hoja Ya Kutokuwa Na Imani Na  Gavana Sonko Kupitishwa Hiyo Jana Ambapo Wakilishi Wadi  88 Waliunga Mkono Hoja Hiyo Huku Wawili Wakipiga Kura Kumuunga Mkono.

Sonko Anatuhumiwa Kwa Matumizi Mabaya Ya Ofisi, Ukiukaji Mkubwa Wa Katiba Na Utovu Wa Nidhamu.

Itakumbukwa Kuwa Gavana Sonko Alikataa Kuidhinisha Bajeti Ya Mamlaka Ya Huduma Za Jiji La Nairobi NMS Akisema Kuwa Hakuna Sheria Inayotengea NMS Shilingi Bilioni 27  Kwa Bajeti Ya Shilingi Bilioni 37.5 Jambo Linalotajwa Kuwa Chanzo Cha Mzozo Kati Yake Ya Wawakilishi Wadi.

Hoja Ya Kumfurusha Sonko Iliwasilishwa Na Kiongozi Wa Wachache Michael Ogada.

Gavana Huyo Atalazimika Kufika Mbele Ya Maseneta Kujitetea  Huku Maseneta Hao Wakiwa Na Jukumu  La Kuamua Hatma Ya Gavana Sonko.

 

Subscribe to eNewsletter