Local Bulletins

Mutunga Samuel akabidhiwa rasmi ofisi za kamanda wa polisi kaunti ya marsabit.

Na Jillo Dida.

Kamanda mpya wa polisi jimbo hili Mutunga Samuel amekabidhiwa rasmi majukumu ya ofisi na mtangulizi wake Ambrose Steve Oloo katika dhifa fupi iliyofanyika katika makao Makuu ya Polisi leo asubuhi.

Oloo ambaye amehudumu kaunti ya Marsabit kwa miezi 16 sasa amepata uhamisho baada ya kupandishwa cheo kuwa Naibu Kamanda wa eneo la Kaskazini Mashariki.

Ambrose Steve Oloo akimkabithi Mutunga Samuel. Photo Credit: Jillo Dida

Akikabidhi mamlaka kwa mrithi wake, Oloo amewataka watumishi wote wa serikali na wakazi kwa jumla kumpa Mutunga mkono wa ushirikano wa kutekeleza majukumu yake mapya.

Aidha, Oloo ameomba msamaha kwa yeyote aliyekosa kumpa huduma anayostahili akisema pia yeye ni binadamu na hana uwezo wa kutosheleza matarajio ya kila mtu.

Vile vile Oloo amesikitikia mauaji yanayoshuhudiwa Marsabit kwa kutaja kuwa ya kinyama.

Amesema kuwa maisha yote ni muhimu na hakuna mtu yeyote anafaa kuaga dunia mikononi mwa binadamu mwenzake.

Kwa maana hiyo amewataka wakazi wa Marsabit kukumbatia amani.

Video: Radio Jangwani

Kwa upande wake Kamanda mpya wa Marsabit Mutunga Samuel amemshukuru mtangulizi wake na kuahidi kuendeleza kazi alikoachia Oloo.

Mkuu huyo wa usalama ameomba pia ushirikiano kutoka wadau wote katika kaunti hii ya Marsabit ili kupata suluhu mwafaka kwa suala la utovu wa usalama.

Insert Samuel ushirikiano.

Mutunga ameongezea kuwa inashangaza kuona katika karne ya 21 watu wangali wanaendelea kumwaga damu ya wasio na hatia.

Amevitaka pia vyombo vya habari haswa radio katika kaunti ya Marsabit kuwa mstari wa mbele kupeperusha matangazo na vipindi kuhamasisha umma kuhusu haja ya kuishi kwa amani.

Kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Mutunga Samuel. Photo Credit: Jillo Dida.

Subscribe to eNewsletter