Local Bulletins

Maridhiano Kati ya Borana na Gabra, watoto waliotoweka warejeshwa salama

Watoto waliotoweka na kisha kupatikana. Picha Jillo Dida.

Na Jillo Dida 3RD JUNE.
Katika hatua ya kuonyesha maridhiano, umoja na upendo kati ya jamii ya Gabra na Borana, watoto wawili kutoka jamii ya Borana hii leo wamekabidhiwa jamii ya Gabra katika hafla ambayo imefanyika kwa furaha kule Bubisa kaunti ndogo ya North Horr hapa Marsabit.
Watoto hao wenye miaka 7 na 11 mtawalia walitoweka wakichunga mifugo wao siku ya Jumanne na kupatikana eneo la Horender.
Chifu wa Horender Abdub Adano Ganya alikabidhiwa watoto hao naye akwakabidhi kwa wazee wa jamii ya Gabra na kisha kupiga ripoti kwa polisi.


Watoto hao wa Kiborna mmoja anatokea kutoka kata ndogo ya jirime naye mwenzake akitokea nagayo, zilizoko wadi ya central eneo bunge la saku.
Akikawabidhi wazeed wa Kiborana watoto hao naibu kamshna wa kaunti ya Marsabit Festus Chepkwony amepongeza hatua hiyo ya jamii ya Gabra akitaja kuwa mfano bora wa kuonyesha maridhiano kati ya jamii hizo mbili ambazo wakati mwingine huwa na mzozo.
Chepkwony pia amewashukuru wakazi wa Bubisa kwa ushirikiano wao waliouonyesha na kusaidia kupatikana kwa watoto hao wakiwa salama.
Nao waliokuwepo wakati wa hafla hiyo, hawakuficha furaha zao, wametaja hatua hiyo kama kitendo cha huruma na kitasalia kama kumbukumbu njema ya mahusiano kati ya jamii hizo mbili.
Wakiongozwa na mzee Pius Yatani jamii ya Gabra wametaja hatua hiyo kuwa msingi bora wa ujenzi ya mahusiano bora baina ya jamii hizo mbili ambazo kwa muda sasa zimekuwa zikizozania maswala ya mbalimbali ikiwemo swala tete la mpaka.
Akizungumza kwa niaba ya Jamii ya Borana, mwenyekiti wa baraza la jamii hiyo Gurach Boru ameshukuru jamii ya Gabra akitaka kutoka pande zote kushiriki mazungumzo kutafuta suluhu la kudumu kwa kero la mitafaruku baina ya jamii.


Kwa upande wake naibu gavana wa jimbo hili Solomon Gubo Riwe amepongeza kitendo hicho akisema ni ishara ya maridhiano ya Amani baina ya jamii ya Gabra na Borana.
Gubo amesema kuwa serikali ya kaunti ya marsabit imejitolea kuunganisha jamii ya Marsabit japo juhudi zao za awali zilionekana kutofaulu.
Naye mwakilishi wa wadi ya central Hassan Jarso amewapongeza wakaazi wa bubisa na jamii ya Gabra kwa ujumla kwa hatua hiyo ambayo ametaja kama ya huruma na ukarimu.

Wazee wa jamii ya Gabra pamoja na Borana katika hafla hiyo kule Bubisa. Picha Jillo Dida.


Mkutano huo uliwaleta viongozi wa serikali ya kaunti ikiongozwa na mwakilishi wa serikali kuu Naibu kamishna Festus Chepkwony, Naibu Gavana wa jimbo hili Solomon Gubo Riwe na mwenyekiti wa baraza la jamii ya borana, wazee wa Gabra na Borana, na wakaazi wa bubisa.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter