Local Bulletins

Madaktari Waitaka Serikali Kuilipa Gharama Ya  Matibabu Ya Daktari Stephen Mogusu Alieaga Dunia Hiyo Jana  Kwa Ajili Ya Korona. 

Daktari Stephen Mogusu Alieaga Dunia Kwa Ajili Ya Korona.Picha :Hisani

By Waihenya Isaac,

Mwenyekiti Wa Muungano Wa  Madaktari Nchini  KMPDU Dr. Samuel Oroko Ametaka Serekali Kuchukulia Kwa Maanani Wahudumu Wa Afya Nchini Ili Kuwaepusha Na Hatari Inayowakondolea Macho Ya Maambukizi Ya Korona.

Akizungumza Jijini Nairobii Oroko Ametaja Kuwa Ni Jambo La Kughadhabisha Mno Kuona Kuwa Serekali Bado Inaendeleza Ajenda Ya Mchakatato Wa Kubadilisha Katiba Mwaka Wa 2020 Huku  Wahudumu Wa Afya Wakikosa Malipo.

Hata Hivyo Oroko Ameweka Bayana Kuwa Wengi  Wa Wahudumu Waafya Wanahatarisha Maisha Yao Kwa Kufanyia Kazi Katika Mazingira Hatari.

Vilevile Madaktari Wameitaka Serikali Kuilipa Gharama Ya  Matibabu Ya Daktari Stephen Mogusu Alieaga Dunia Hiyo Jana  Kwa Ajili Ya Korona.

Daktari Huyo Mwenye Umri Wa Miaka 28  Alikuwa Akihudumu Katika Kituo Cha Kutibu Covid 19 Huko Machakos Ambako Aliambukizwa Virusi Hivyo.

Inaarifiwa Kuwa  Gharama Ya Matibabu Yake Ilikuwa Imefika Shilingi Laki Nane.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter