Local Bulletins

Maafisa wa polisi Marsabit wapokea mafunzo dhidi ya Covid 19.

Idara ya usalama kaunti ya Marsabit imepigwa jeki katika suala la kupokea elimu na hamasisho kuhusiana na kero la ugonjwa wa covid 19 nchini.

Akizungumza na wanahabari mwishoni mwa juma mjini Marsabit  baada ya kufanya kikao na wawakilishi wa Muungano wa Chama Cha Wamiliki Bunduki nchini (NGOA) kamanda wa polisi Samuel Mutunga alisema kuwa maafisa wake zaidi ya 90 wamepokea mafunzo ya kujikinga dhidi ya corona wakiwa kazini ikiwemo kupewa vifaa vya kunyunyizia dawa ya kuuwa virusi kwenye magari ya polisi sawia na kusafisha  bunduki zao.

Maafisa waliopokezwa mafunzo hayo ni wale kutoka maeneo ya Moyale, Turbi, Marsabit Mjini, Sololo na Laisamis

Aidha Kamanda Mutunga ametoa wito wa wananchi kujilinda kwa kufuata sheria za wizara ya afya pasi na kulazimishwa na maafisa wa polisi akisema kuwa vita hivi dhidi ya corona vitawezekana wananchi wakifuata masharti.

Mwenyekiti wa chama cha wamiliki bunduki nchini kanda ya Mlima Kenya Mustafi Isaac na ambaye anaongoza hamasisho dhidi ya ugongwa wa covid 19 amesema kuwa muungano wao umekuwa ukifanya hamisisho kwa maafisa wa  polisi dhidi ya uwepo wa corona ambapo kufikia sasa wametoa mafunzo kwa zaidi ya maafisa wa polisi zaidi ya elfu saba katika kaunti 33.

Ameongeza kuwasema kuwa polisi wapo mstari mbele kwenye mapambano dhidi ya corona hivyo kuna haja ya kupewa elimu na namna ya  kujikinga wakiwa kazini.

Subscribe to eNewsletter