Local Bulletins

COG Yaagiza Mishahara Ya Wahudumu Wa Afya Wanaogoma Kusitishwa Na Hatua Za Nidhamu Kuchukuliwa.

Mwenyekiti Wa Baraza La Magavana Nchini Wycliff Oparanya. Picha: Hisani

By Waihenya Isaac
Baraza La Magava COG Limeshauri Serekali Zote Za Kaunti Humu Nchi Kusistisha Ulipaji Wa Mishahara Ya Wahudumu Wa Afya Wanaoendelea Na Mgomo Na Kuchukua Hatua Za Nidhamu Dhidi Ya Wale Hawajafika Kazini.
Kwenye Arafa Iliyotumwa Kwenye Vyombo Vya Habari, COG Kupitia Mwenyekiti Wake Wycliff Oparanya Inataka Serekali Zote Za Kaunti Kutanganza Nafasi Zilizowachwa Wazi Na Madaktari,Wauuguzi Pamoja Na Wahudumu Wa Afya Wanaogoma.
Baraza Hilo Limekariri Kuwa Bado Mgomo Unaoaendelea Ni Haramu Na Kuilaumu Miungano Mbali Mbali Ya Wahudumu Wa Afya Kwa Kukosa Kutii Agizo La Mahakama Na Kuwaagiza Wahudumu Wa Afya Kurejea Kazini.
Kaimu Katibu Mkuu Wa Chama Cha Madaktari Nchini KMPDU Daktari Mwachoda Chibanzi Amewataka Madaktari Kutorejea Kazini Na Kuitaja Barua Ya Baraza La Magavana Nchini COG Kama Vitisho.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter