Local Bulletins

Chris Obure apata pigo Mahakani.

Na Waihenya Isaac

MAHAKANI BY WAIHENYA 4PM……………….

Mshukiwa kwenye mauaji ya Kevin Omwenga,Chris Obure amepata pigo baada ya mahakama kutupilia mbali  ombi lake la kutaka kufanywa kuwa shahidi badala ya kuwa mshukiwa kwenye mauji hayo.

Akitoa uamuzi kwenye kesi hiyo Jaji Mumbi Ngugi ameamuru kuwa ombi la mshukiwa huyo halina misingi na Kuwa  mahakama haina ruhusa ya kuuamulia upade wa mashtaka kuhusu ni nani anafaa kuwa mshukiwa au shahidi.

Aidha Mahakama hiyo imesema kuwa uamuzi kuhusiana na swala  hilo utatolewa wakati wa kuendelea kwa kesi hiyo kwa kuzingatia ushahidi utakaowasilishwa.

Obure alikuwa amekataa kula kiapo kwenye kesi hiyo na badala yake kutaka abadilishwe na kuwa shahidi kwenye mauaji hayo yaliyotokea  tarehe 21 mwezi Agosti  mwaka huu katika eneo la kilmani jijini Nairobi.

Subscribe to eNewsletter