Local Bulletins

Baraza La Magavana Lawataka Wahudumu Wa Afya Kurejea Kazini.

Baraza La Magavana Nchini Wycliff Oparanya. Picha: Hisani

Na Waihenya Isaac,

Huku Mgomo Wa Wahudumu Wa Afya Ukiingia Siku Yake Ya Nne Hii Leo, Baraza La Magavana Nchini Limetataka Magavana Wote Wakutane Na Vyama Vya Wafanyakazi Vya Afya Vya Kaunti Vinavyotambuliwa Na Kujadili Malalamiko Yao Kwa Nia Ya Kutatua Malalamishi Ya Wafanyikazi Wa Afya Kwa Amani.

Kwenye Taarifa Kupitia Mwenyekiti Baraza Hilo Wycliff Oparanya Ni  Kuwa  Serekali Za Kaunti Hazijapokea Zaidi Ya Shilingi  Bilioni 60 Ambazo Ni Mgao Wa Kila Mwezi Wa Mwezi Oktoba, Novemba Na Desemba.

Oparanya Amesema  Kuwa Imekuwa Vigumu Kulipa Hata Mishahara Ya Wafanyikazi Na Hivyo Kuwataka Wahudumu Wa Afya Kuelewa Hali Hiyo Na Kurejea Kazini.

Amesema Kuwa Kenya Kama Mataifa Mengine Inakumbwa Na Changamoto Za Kiuchumi Haswa Wakti Huu Wa Janga La Korona.

Pia Amewataka Wahudumu Wa Afya  Kuheshimu Hatua Ya Mahakama Ya Viwanda Na Wafanyikazi Ya Kuwataka Kusitisha Mgomo Wao.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter