Local Bulletins

Afueni Kwa Wakaazi Wa Maeneo Ya Garma Kaunti Ya Samburu Baada Ya Serekali Ya Kaunti Kuzindua Kisima Cha Maji.

Kisima Cha Maji Katika Kaunti Ya Samburu.
Picha; Hisani.

By Waihenya Isaac.

Wakaazi Wa Maeneo Ya Garma  Pamoja Na Vijiji Jirani  Katika Kaunti Ndogo Ya Samburu Ya Kati Wanakila jambo la Kutabasamu  Baada Ya Safari Ndefu Wazikuwa Wakitembea Wakitafuta Maji Kufupishwa.

Hii Ni Baada Ya Serekali Ya Kaunti Ya Samburu Kwa Ushirikiano Na Hazina Ya Maji Katika kaunti Hiyo  Kuzindua Kisima Cha Maji Kinachogarimu Shilingi  Millioni Sabini Na Saba Ambacho Kitatumiwa Na  Zaidi Ya Wakaazi  Elfu Kumi Na Tisa Katika Vijiji Tofauti.

Baadhi Ya Wenyenji Wa Eneo Hilo Walielezea  Furaha Yao Baada Ya Kurahisishiwa Kuipata Bidhaa Hiyo Adimu.

Aidha Meneja Mkurugenzi  Wa Kampuni Ya Kusambaza Maji  Katika Kaunti Ya Samburu SAWASCO Mark Lenolkulal Amesema Kuwa  Maeneo Yatakayonufaika Ni Garma,Morgur, Loosho, Lokuru, Suradoru Negrupos Na Lodokojek Samburu Ya Kati.

Kadhalika Kamishna Wa Kaunti Ya Samburu John Korir Amewahimiza Wenyeji Kutunza Kisima Hicho Huku Akiwarai Wananchi Kudumisha Amani Kama Njia Moja Wapo Ya Kuimarisha Ukuaji Wa Uchumi Wa Kaunti Hiyo.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter