Local Bulletins

Na Adho Isacko

Kamishna wa kaunti ya Marsabit Evans Achoki amesema kuwa Uchunguzi umeanzishwa ya kuwakamata wahalifu waliowaua watu wawili siku ya jumatano 27-5-2020 katika eneo la Gof Choba.

Achoki amelaani kitendo hicho akidai kuwa kuna malisho ya kutosha kwa sasa na hivyo hakuna haja ya wafugaji kupigania malisho kwa sasa.  

Achoki ameongeza kuwa kila lokesheni katika kaunti ya marsabit itakuwa na kamati ya kushugulikia maeneo ya malisho ili kuwe na mpangilio katika jamii wanapoenda kulisha mifugo zao.

Ameongeza kuwa tayari wameagiza machifu kuunda kamati za kushugulikia maeneo za malisho ili kusiwe na mizozo kati ya jamii.

Achoki pia aliwahimiza viongozi kulaani mambo ya uchochezi ambayo mara kwa mara yanaleta vifo katika jamii.

Kati ya mikakati ambayo wameanzisha kwa sasa ili kuzuia vita vya kijamii ni kama vile kuweka maafisa wengi wa kushika doria katika sehemu zenye utata, kuweka mikutano ya amani ili kujadiliana na jamii na kukomesha vita, mikutano na viongozi kama vile machifu ili kuleta pamoja jamii na viongozi wao ili uhasama ulio katika kaunti hii itatuliwe.  

Kuhusiana na mwalimu aliyepigwa risasi usiku wa jumanne, Achoki alisema kuwa, wanachunguza kisa hicho ili kumkamata mshukiwa.

Aliwahimiza wakaazi kushirikiana na polisi ili kushika wahalifu na viongozi ambao wanachochea jamii.

Subscribe to eNewsletter