Local Bulletins, Machapisho ya Kiswahili

Mo Salah anaweza Kushiriki Olimpiki mwaka ujao.

Mo Salah akiichezea timu ya Misri.
Picha: Hisani.

Na Waihenya Isaac.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Misri chini ya umri wa miaka 23 Shawky Gharib, amesema ni mapema mno kutangaza maamuzi ya kumjumuisha mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah, kwenye kikosi chake kwa ajili ya michuano ya Olimpiki 2020, itakayofanyika mjini Tokyo, Japan.


Tayari Misri imeshafuzu kushiriki michuano hiyo, kwa kutinga hatua ya fainali ya mashindano ya Afrika chini ya umri wa miaka 23, itakayofikia tamati kwa wenyeji kupambana na Ivory Coast.


Kanuni za michuano ya Olimpiki zinatoa nafasi kwa kila timu shiriki kuwatumia wachezaji watatu waliozidi umri wa miaka 23, na tayari mashabiki wa soka nchini Misri wameanza kumshawishi kocha Gharib kutomsahau Mohamed Salah.

Nembo ya Olimpiki 2020.
Picha: Hisani

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter