Mwanaume mmoja mweye umri wa miaka 24 afariki baada ya kugongwa na nyaya za umeme katika eneo la Dirib Gombo.
February 27, 2025
Na Joseph Muchai,
Wito wa kupambana na dawa za kulevya miongoni mwa vijana umetolewa kwa wakaazi wa kaunti ya Marsabit. Akiongea na meza ya habari ya Radio Jangwani, mchungaji wa kanisa la Kenya Assemblies of God (KAG)Marsabit mjini Reverend Joseph Mwenda amewataka washikadau wote kushirikiana na kuhakikisha kuwa uozo huo unakomeshwa ili vijana wapate nafasi ya ukuaji kwa njia inayofaa.
Aidha mchungaji Mwenda amewataka wanaousika katika kuhakikisha kuwa utumizi wa mihadarati unakomeshwa kusimama tisti bila kuyumbishwa na chochote ili kuhakikisha usalama wa vijana na watoto umeimarishwa dhidi ya dawa za kulevya.
Aidha kiongozi huyou wa kidini amesikitikia jinsi dawa za kulevya kwa sasa zinatumika hata na watoto wa shule huku watu wenye jukumu la kuzuuia tatizo hilo wakitazama kimyakimya.
Vile vile amewataka wazazi kuhakikisha kuwa wanawachunga wanao kwa kuchunguza mienendo yao ili wasije wakajiingiza kwenye tatizo hilo.
Wakati uohuo mchungaji Mwenda amewarai wakaazi kuiombea nchini na jimbo la Marsabit haswa wakati huu ambapo swala la mihadarati limesalia kuwa kero.
Haya yanajiri huku utumizi wa dawa za kulevya miongoni mwa vijana na watoto walio nchini ya umri wa miaka kumi na mitano ukiripotiwa kuongezeka siku za hivi karibuni hapa nchini.