Mwanaume mmoja mweye umri wa miaka 24 afariki baada ya kugongwa na nyaya za umeme katika eneo la Dirib Gombo.
February 27, 2025
Na Samuel Kosgei
IDARA ya maji kaunti ya Marsabit imetakiwa kutia juhudi kuhakikisha kuwa inatoa suluhu la kero ya maji katika sehemu ambazo zinashuhudia ukosefu wa maji jimboni Marsabit.
Mkurugenzi wa shirika la lisilo la kiserikali Kenya Drylands Education Fund (KDEF), Ahmed Kura akizungumza na kituo hiki kwenye kipindi Cha Amkia Jangwani leo asubuhi alisema kuwa matatizo mengi ya maji katika kaunti ya Marsabit yanaweza kusuluhishwa kupitia ushirikiano wa mashirika yasiyo ya serikali na serikali ya kaunti.
Ameondolea lawama wawakilishi akidai kuwa kero kuu ni idara yenyewe ya maji ambayo inajikokota kutoa suluhu ya kudumu.
Kauli yake imejiri huku akijibu kuhusu habari tuliyoifanya jana Jumatano kuhusu mahangaiko wanayopitia wakaazi wa Karare, eneobunge la Saku baada ya kisima chao kuharibika na pia ndovu kuharibu mifereji ya maji katika eneo la Bongole.
Kura ameahidi kuwa shirika la KDEF litarekebisha matatizo kwenye kisima hicho walichokichimba katika eneo hilo ili kunusuru mahangaiko wanayopitia wananchi wa eneo hilo. Anasema suala litakuwa limeshughuliliwa kufikia katikati ya mwezi ujao.