Mwanaume mmoja mweye umri wa miaka 24 afariki baada ya kugongwa na nyaya za umeme katika eneo la Dirib Gombo.
February 27, 2025
Na Caroline Waforo,
Serikali imeweka mikakati kuhakikisha kuwa wanafunzi wote katika eneo bunge la Laisamis kaunti ya Marsabit wanapata vyeti vya kuzaliwa ili kuwawezesha kupata huduma mbalimbali kutoka kwa serikali kuu ikiwemo ufadhili wa elimu kwa kuhakikisha kuwa wamesajiliwa katika mfumo wa NEMIS.
Haya ni kulingana na naibu kamisha wa eneo bunge hilo la Laisamis Kepha Maribe ambaye amezungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu.
Maribe amesema kuwa wanaendelea na zoezi la kuwasajili watoto ili kufanikisha upatikananji ya vyeti vya kuzaliwa.
Na huku wazazi wakizidi kutakiwa kuwajibika katika malezi ya wanao DCC Maribe ametoa wito kwa wazee vijijini kuhakikisha kuwa watoto hawawajibishwi katika kazi sulubu au hata shughuli za kuchunga mifugo maeneo ya mbali.
Aidha DCC Maribe amesisitiza kuwa wanaendelea na kuwasajili wananchi katika bima mpya ya Taifa Care chini ya mamlaka ya afya ya jamii SHA.