Mfumo wa kutatua kesi nje ya mahakama (AJS) wazinduliwa rasmi,Marsabit.
November 23, 2024
Na Grace Gumato
Shughuli za masomo na biashara zimeadhirika katika eneo la Balesaru na Dukana kutokana na mzozo wa mipaka katika taifa la Kenya na taifa njirani la Ethiopia.
Wakizungumza katika kikao cha usalama kilichowaleta pamoja jamii zinazoishi kwenye mipaka wakaazi wa eneo hilo wakiongozwa na mwakilishi wa akina mama ni kuwa shule zimesalia kufungwa kutokana na ukosefu wa usalama katika eneo hilo kwa muda wa wiki mbili zilizopita na huku hali ya usalama ikizidi kuimarishwa.
Aidha mzee Ali Adano ambaye ni mzee katika eneo hilo amesema kuwa hakuna askari wa kutosha eneo la Dukana na hivyo kutaka serikali kuajiri askari wa akiba NPR ili kuwasidia katika kupiga jeki swala la usalama.
Hata hivyo wakaazi hao wameiomba serikali za kitaifa na mashirika mbali mbali kuwapa chakula wakisema kuwa mifugo waliokuwa wakitegemea zimeisha kutokana ukame mwaka ulio pita.