Mfumo wa kutatua kesi nje ya mahakama (AJS) wazinduliwa rasmi,Marsabit.
November 23, 2024
NA ISAAC WAIHENYA
Kulingana na walimu wakuu katika badhi ya shule za msingi za umaa tulizozuru hii leo ni kuwa asilimia kubwa ya wanafunzu hawajaripoti shuleni siku ya kwanza kutokana na mgomo wa walimu wa uliokuwa umetangazwa na chama cha walimu nchi KNUT na kisha baadae kufutwa dakika za mshisho.
Wakiongozwa na mwalimu mkuu katika shule ya msingi ya Marsabit, Abdi Anno walimu wakuu hao wametaja kwamba idadi ya wanafunzi waliofika shule humo imo chini mno huku baadhi ya madarasa yakiwa hayana hata mwanafunzi mmoja.
Kauli yake inakaririwa na naibu mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya SKM Bi. Ruth Lekesike ambaye ametaja kwamba ni asilimia 30 pekee ya wanafunzi katika shule hiyo walioripoti shuleni hii leo.
Hata hivyo hali tofauti ilishuhudiwa katika shule ya msingi ya Alhidaya ambapo mwalimu mkuu wa shule hiyo Hirbo Barisso ametaja kwamba wanafunzi 524 kati 720 wameripoti shuleni hii leo.